Majukumu ya kitengo cha TEHAMA ni kama ifuatavyo:-
• Kuweka mahusiano bora baina ya Halmashauri pamoja na Umma na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa Umma.
• Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta(System Administration)
• Usimamizi wa Mtandao wa Kompyuta pamoja na vifaa vyake (Network and Hardware Adminstration).
• Usimamizi wa Benki Ya Takwimu (Database Administration)
• Kuandaa machapisho mbalimbali ya Halmashauri.
• Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails).
• Kutekeleza sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
• Kuandaa mahitaji katika Ununuzi wa vifaa vya TEHAMA.
NB: Lengo kuu la kitengo hiki ni kuhakikisha miundombinu ya TEHAMA katika Halmashauri inakuwa bora na salama katika utoaji wa huduma(taarifa).
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Kitengo kimejiwekea malengo yafuatayo:-
• Kushauri kitaalam katika manunuzi ya vifaa bora na vya kudumu vinavyohusu TEHAMA.
• Kuendelea Kuboresha miundombinu ya TEHAMA ifikapo 30, Juni 2018.
• Kuweka usalama wa hifadhi data.
• Kutoa huduma za hifadhi data kwa watumiaji.
• Kusimamia maboresho ya programu za kompyuta kwa wakati.
• Kusakinisha, kusanidi na kuboresha programu za kuzuia virusi vya kompyuta. (Install, configure and update antivirus software).
• Kuelimisha watumiaji masuala mbalimbali yanayohusu usalama, hatari na udhaifu katika mifumo ya TEHAMA.
• Kukagua mifumo ya TEHAMA mara kwa mara.
• Kuweka viwango vya usalama na udhibiti katika mifumo ya TEHAMA kwa watumiaji.
• Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa kompyuta (Desing, install and configure LAN and WAN infrastructure).
• Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa kompyuta.
• Kutengeneza vifaa vyote vya TEHAMA vinapoharibika au kutofanyakazi iliyokusudiwa kwa kupitia kwa fundi sanifu wa Kompyuta.
• Kusimamia mifumo ya kompyuta hasa mifumo ya Mapato na Mashine za Kukusanyia Mapato (Point Of Sales - POS).
• Kuimarisha ufanisi wa ufanyaji kazi wa kompyuta kwa kufanya matengenezo ya mara kwa mara ifikapo Juni 30, 2018.
• Kuwaelekeza watumiaji namna sahihi ya kutumia kompyuta ili ziweze kudumu kwa muda mrefu ifikapo Juni 30, 2018.
• Kuongeza mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato na kufikia angalau 35 ifikapo June 30, 2018.
• Kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi na haraka zenye ufanisi kwa kutumia tovuti na barua pepe za serikali kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara/Vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wialaya Kasulu ifikapo Juni 30, 2018.
Mwongozo wa Matumizi Bora na Salama ya TEHAMA
Waraka wa Utumishi Na. 5 Kuhusu - Mwongozo wa Matumizi Bora na Salama ya TEHAMA
Check on the followning video:
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.