HISTORIA FUPI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU.
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ni kati ya Halmashauri nane zinazounda Mkoa wa Kigoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ni Mheshimiwa Eliya C. Kagoma na Mkurugenzi Mtendaji ni Ndg.Joseph Kashushura Rwiza.
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ina eneo lenye ukubwa wa KM 5324 za mraba. Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ina idadi ya watu 537,767.
Shughuli za kiuchumi za wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ni kilimo, ufugaji ambapo kwa upande wa kilimo, mazao ya mahindi na maharage ndio mazao makuu ya chakula na zao la tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara.
Zao la mhogo pia hulimwa kwa wingi na hutumika kwa chakula na biashara kama yalivyo mazao ya mahindi na maharage.
Kwa upande wa ufugaji wakazi wa wilaya ya Kasulu wanafuga mifugo mbalimbali ikiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo kukiwa na muingiliano mkubwa wa wakulima na wafugaji kutoka maeneo mengine ndani na nje ya nchi wanaokuja kutafuta ardhi ya kilimo na malisho ya mifugo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.