Na Mwandishi Wetu
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma za kibingwa zinazotolewa na madaktari bingwa walioweka kambi katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa gharama nafuu.
Wito huo umetolewa leo hospitalini hapo na Kiongozi wa Timu hiyo, Dkt. Agustino Maufi, ambaye amewataka wananchi kutoendelea kubaki majumbani iwapo wanakabiliwa na changamoto za kiafya, kwani huduma hizo zimesogezwa karibu ili kupunguza gharama na adha ya kuzifuata mbali.
Kwa upande wake, Tabibu wa Afya ya Kinywa na Meno wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, Zera Ambonisye, amesema kambi hiyo imemsaidia kuongeza ujuzi katika kutoa tiba ya kuua fahamu ya mshipa wa jino na kusoma picha za X-Ray kwa usahihi.
Naye mmoja wa wananchi walionufaika na huduma hizo, Rojasi Kayeke kutoka Kijiji cha Chekenya, ameiomba Serikali iwapo madaktari hao watarudi kwa mara nyingine basi muda wa utoaji huduma uongezwe kutoka siku tano hadi angalau kumi, kutokana na mahitaji makubwa ya wananchi hususan wa vijijini kupata huduma za kibingwa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.