Baadhi ya Viongozi walioshiriki Mkutano wa Baraza kujadili makisio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/202. Kutoka Kushoto ni Katibu wa CCM(W) Ndg.Mashaka Mshora, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kan. Simon Anange, Diwani Kata ya Rusesa Mhe. Fabiano Doragi, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Yohana Mshita, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya mwishoni ni Mhe.Josephine Genzabuke Mbunge viti Maalum Mkoa wa Kigoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mha. Godfrey Kasekenya(kulia) Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Yohana Mshita (katikati) na Diwani wa Kata ya Rusesa Mh. Fabiano Doragi wakiwa katika Picha ya pamoja kabla ya kuanza Mkutano wa Baraza kujadili Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.Baadhi ya Wah. Madiwani wakifuatilia uwasilishwaji wa makisio ya Bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Kasulu kwa Mwaka 2019/2020 kwenye Ukumbi wa Halmashauri.
Na.Andrew Mlama.
Baraza la Madiwani wa Halamshauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma limepitisha Mapendekezo ya Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 yenye makisio ya zaidi ya Shilingi bilioni 48.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akiwasililisha Bajeti hiyo, Afisa Mipango Takwimu na ufuatiliaji wa halmashauri Ndg. Jackob Kilatu, amesema ili kukidhi mapendekezo hayo halmshauri inatarajia kukusanya kiasi hicho cha Fedha kutoka Serikali kuu na vyanzo mbalimbali vya Mapato ya ndani ya halmashauri hiyo pamoja na wadau wa maendeleo.
Bajeti hiyo imejielekeza zaidi katika Elimu Afya na Maji kwa kukamilisha miradi ambayo iliyoanza kutekelezwa na haijakamilika pamoja na miradi mipya iliyoibuliwa na wananchi katika kata 21 za halmashauri.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.