Na Mwandishi Wetu
Katika kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwenye shughuli za Mwenge wa Uhuru pamoja na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imepanga kuandaa Bonanza kubwa la Michezo litakalofanyika Jumamosi, Septemba 6, 2025.
Akizungumza leo, Jumatatu Septemba 1, 2025, katika kikao cha maandalizi ya Mwenge kilichokutanisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu, amesema bonanza hilo litakuwa chachu ya mshikamano wa wananchi kuelekea matukio hayo muhimu ya kitaifa.
“Bonanza letu litafanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiganamo na litajumuisha michezo mbalimbali. Wananchi wote wanakaribishwa kushiriki, ambapo tutaanza na matembezi ya pamoja kuzunguka maeneo ya Kasulu mjini kisha kurejea viwanjani kwa michezo na shughuli za kijamii zitakazowaunganisha watu wa kada zote,” amesema Mhe. Mwakisu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.