Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Rukia Adam Bakari amewataka wazazi kutokatisha masomo ya watoto na kuwaingiza katika shughuli za kutafuta fedha ili kuzihudumia familia zao
Aliyasema hayo alipokuwa kwenye hafla ya kusherekea siku ya kuzaliwa kwa watoto wanaofadhiliwa na Shirika la World Vision Tanzania kupitia Mradi wa BUHOMA unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
“Wazazi tuache tamaa tupeleke watoto shule badala ya kuwafanya vitega uchumi kwa kuwapeleka kwenye utumishi wa kazi za ndani ili kuleta fedha kwaajili ya sisi wazazi”.
C7756AED-2945-4332-9811-F9C435EA70C1.jpeg
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Bi. Subira Swai alitoa rai kwa wazazi kukaa karibu na watoto kama njia moja ya kuhimiza malezi chanya badala ya kujikita kwenye shughuli za uzalishaji muda wote na kuwaacha kujilea
Sambamba na hayo Shirika la WVT kupitia mradi wa BUHOMA unaotekelezwa katika vijiji 10 vilivyopo katika halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limetoa zawadi ya kadi za bima ya afya, viatu na blanketi kwa watoto wanaofadhiliwa na mradi huo
Hii ni katika kuletekeleza mkakati wa miaka mitano 2021-2025 wa shirika hilo wa kuhakikisha kila mtoto anakuwa na afya nzuri na kufurahia maisha katika utimilifu wake.
Aidha zawadi hizo zimetolewa kuwa sehemu ya kumbukumbu za siku za kuzaliwa kwa watoto hao ikiwa ni alama ya kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika mwaka mwingine wa kuishi na kuonja upendo wake na majirani zao
Zawadi hizi zinajumuisha kadi za bima ya afya kwa watoto 100, viatu vya shule kwa watoto 600 na blanketi za kulalia kwa watoto 1,650. Zawadi hizi zina jumla ya thamani za shilingi za Kitanzania 90,990,000/=
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.