Na Mwandishi Wetu
Makarani waongozaji wapiga kura katika Jimbo la Kasulu Vijijini wametakiwa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa, kwa kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na mawakala wa vyama watakaokuwepo vituoni, kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Wakili Emmanuel Ladislaus, ametoa wito huo leo Jumamosi, Oktoba 25, 2025, wakati akifungua Semina ya Uchaguzi kwa makarani hao katika Chuo cha Ualimu Kasulu (TCC) mkoani Kigoma.

“Fanyeni kazi kwa ushirikiano kama timu ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na ufanisi. Hakikisheni mnafika mapema vituoni ili kukamilisha maandalizi kabla ya muda rasmi wa upigaji kura, yaani saa 1:00 kamili asubuhi,” amesema Wakili Ladislaus.

Aidha, amewataka makarani hao kuzingatia taratibu zote za utoaji wa taarifa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi pekee, pamoja na kutekeleza kwa uaminifu viapo vyao vya kutunza siri na kutokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa kipindi chote cha uchaguzi.
Sem
ina hiyo imehusisha makarani waongozaji wapiga kura kutoka vituo 552 vya kupigia kura vilivyopo katika kata 21 za Jimbo la Kasulu Vijijini, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2025.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.