Wananchi wa Wilaya ya kasulu wamehaswa kudumisha amani iliyopo kwatika nchi ya tanzania ili waweze kufanya kazi katika mazingira yasiyo kuwa na matishio kwani uvunjifu wa amani husababisa kukosekana Kwa maendeleo.
aliyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Antony Mwakisu alipokua akiongea na wananchi katika iftari iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya Kasulu pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu na Halmashauri ya Mji Kasulu aprili 19, 2023.
Mwakisu alisisitiza wananchi wa Kasulu kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kisiwa cha amani kwani endapo amani ikitoweka hakuna shughuli yoyote ya uzalishaji mali itafanyika katika maeneo yao.
“Ndugu zanguni amani ikipotea hakuna kinachoendelea niwasihi sana katika hili tudumishe amani yetu tuendelee kuwa kisiwa cha amani najua huko nyuma kulikuwa na shida kidogo katika wilaya yetu kulikua na utekaji na hili wakati tunakuja tulikiongea kwa uwazi
Kwamba nataka vijana wa Kagera Nkanda jioni Ijumaa waje Kasulu Kwa taxii na warudi kwao nakuthibitishia sheikh wale vijana wanakuja na kurudi”, alisema Mwakisu.
Aidha Mwakisu aliwataka wananchi hao kukemea vikali Matendo ya mahusiano ya jinsia moja na kutoyafumbia macho kwani wakionea aibu mambo hayo watatekekeza taifa lao kwa kupelekea kukosa Watu wenye uwezo wa kulitumikia taifa lao.
“Niwaombe Kwa kutumia hadhara hii tuko kwenye vita watoto wetu wanaharibika angalau MUNGU ametupa hekima tumekua Watu wazima tunajitambua wapo watoto wetu ambao ndio wanatafutwa Kwa kiasi kikubwa ili Tanzania yetu ya baadae isiwe na Watu wenye uwezo wa kulitumikia taifa hili”, alisema Mwakisu
Vilevile alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika Wilaya ya Kasulu ambayo imegusa Jamii moja Kwa moja kupitia miradi ya afya, elimu, maji na barabara
Aliongeza kuwa wananchi waendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Kwa kazi nzuri ambayo ameionesha kwani katika miaka yake 22 ya utumishi hakuwai kuona Rais akipeleka hela zinaenda kwenye utekelezaji kama kipindi cha mama SSH.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.