Na Mwandishi Wetu
Afisa Elimu (Taaluma) wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mussa Kanyoe amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Titye kuongeza kiwango cha ufaulu kama Shukrani kwa Rais wa Awamu ya Sita Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mushirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha elimu bila malipo inatekelezeka.
Kanyoe ametoa kauli hiyo leo Mei 31,2024 kwenye hafla ya utoaji magodoro 100 kwenye shule hiyo yaliyotolewa na Umoja wa watu wa Titye waishio mkoani Dar es Salaam.
Ambapo amewapongeza kwa uzalendo mkubwa waliouonyesha kwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia aliyeboresha miundombinu mbalimbali ya kujifunzia mashuleni.
"Walichokifanya ni uzalendo katika taifa mbali na kwamba walisomea katika shule hii ni wachache sana ambao wanakumbuka wametoka wapi katika Halmashauri yetu... we
wiki hii imekua ya bahati sana kwani yupo mtanzania aliejitolea vitabu katika Shule ya Sekondari Nyenge ili kuboresha mazingira ya kujifunza," amesema.
Akiongea kwa niaba ya umoja huo, Levocatus Ntagata amesema wamefanya hivyo ili kuongeza hamasa na kuchochea ufaulu kwa wanafunzi hao na kuwaweka pamoja ili kupata muda wa kushirikiana na kujisomea hasa nyakati za jioni.
Na kuongeza kuwa wakiwa kama wadau wa elimu wana imani magodoro hayo yatatunzwa vizuri ili yatumike kwa wanafunzi wajao na kutoa shukrani kwa halmashauri kukubali kupokea msaada huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Titye, Eden Mkole ameelezea kuwa msaada huo utasaidia kuimarisha miumdombinu ya usomaji na ujifunzaji kwa wanafunzi tofauti na ilivyokua hapo awali.
Kwa upande wake Kaka Mkuu wa shule hiyo, Naftar Leonad ameushukuru umoja huo na kuahidi kuwa watapandisha ufaulu wa shule hiyo kwa kusoma kwa bidii huku akiwaomba wadau hai na jamii kiujumla kuwasaidia ujenzi wa mabweni zaidi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.