Corona ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona katika mwili wa binadamu (COVID-19). Kufikia tarehe 19 Machi nchi 170 zilikuwa na mgonjwa walau mmoja. Jumla ilifikia 227,000 na vifo 9,300 kati nchi 40. Ulaya ilikuwa imezidi China kwa wingi wa vifo. Tarehe 18 Machi nchini Italia walifariki watu 475, kuliko siku yoyote ya China.
DALILI ZA UGONJWA WA CORONA:
Dalili kuu za ugonjwa wa Corona ni pamoja na
Homa kali,
Uchovu
Kikohozi kikavu
kukosa pumzi
Makundi yaliyo kwenye hatari zaidi ni yapi?
WHO (Shirika la Afya Duniani) inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama Shinikizo la Damu, Kisukari, Matatizo ya Figo ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kuathika pindi wanapopatwa na virusi vya Corona. Watu wa umri wa wastani na wenye afya imara wanaweza kupata virusi vya Corona na kupona bila kuhitaji matibabu.
Virusi vya Corona vinasambaa vipi?
Virusi vya Corona vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. Iwapo mtu anagusa maji maji kama mafua, mate na makohozi ya mtu aliye na virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua anaweza kupata virusi vya Corona.
Namna ya Kujikinga na Virusi vya Corona:
Nawa vizuri mikono yako kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu kwa angalau sekunde 20.
Kaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.
Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi.
Hakikisha wewe, na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.
Baki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kwa sababu huko wataalamu watakupatia msaada muhimu
Epuka kuwa sehemu yenye msongamano, kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye yenye mgandamizo wa hewa.
Nunua kifunika mdomo na pua na kukikavaa ukiwa kwenye mikusanyiko.
Fuatilia taarifa za afya na matangazo yake kuhusu virusi vya Corona.
Tiba ya Virusi vya Corona:
Hadi sasa hakuna tiba au chanjo dhidi ya virusi vya Corona lakini kwa sababu virusi hivyo vinaleta dalili mfano wa zile za mafua makali, mchanganyiko wa tiba unatumika kupunguza athari za virusi vya Corona.