Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Rugwa leo Jumatatu Agosti 5,2024 ametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Magharibi yanayoendelea katika Viwanja vya Nane Nane Ipuli mkoani Tabora.
Akizungumza katika tukio hilo Rugwa amesema kuwa amefurahishwa na namna maonesho hayo yanavyoendelea hasa kwa washiriki kutoka Mkoa wa Kigoma kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya na jinsi wanavyotoa elimu kwa umma kuhusiana na teknolojia mbalimbali za kilimo.
“Binafsi nimefurahishwa na ninamkaribisha kila mmoja kutenga muda na kuja kujionea maonesho haya hasa namna teknolojia za kilimo zilivyobadilika…naamini malengo ya nchi kwa sasa kupitia maonesho haya yatatimia kwakuwa washiriki wanaonesha namna teknolojia ya kilimo ilivyopiga hatua kwa maendeleo ya jumla ya taifa letu,” amesema.
Pia, amebainisha kuwa washiriki kutoka Mkoa wa Kigoma kupitia shughuli hiyo wataongeza mnyororo wa thamani wa bidhaa zao pamoja na kuongeza wigo mpana wa ufanyaji wa biashara.
Kupitia tukio hilo Rugwa alipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali za wakulima,wafugaji na wajasiriamali kutoka Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu wenye lengo la kuuza bidhaa na teknolojia zao mbalimbali.
Kauli mbiu ya maonesho hayo kwa mwaka huu ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.