Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi wa Kijiji cha Mvinza kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi baada ya maeneo ya kijiji hicho kupimwa ili uwasaidie kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.
-
Kanali Mwakisu ametoa kauli hiyo jana alipofanya mkutano wa hadhara
kijiji humo kilichopo katika Halamashauri ya Wilaya ya Kasulu alipoenda kutoa maelekezo ya serikali juu ya mgogoro kati ya kijiji cha hicho na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
-
Huku akitawataka kuhakikisha ushiriki wao katika mpango huo ili kuweka mipango bora itakayowasaidia kutumia ardhi kwa usawa.
"Naomba mpokee taarifa hii ukubwa wa kijiji upimwe mpate ramani yenu ili kijiji kisajiliwe na mfanye mpango wa matumizi bora ya ardhi muondokane na migogoro itakayowasaidia kuitumia kwa usahihi", amesema.
-
Pia, ametaadharisha uchukuliwaji wa hatua kali za kisheria kwa watu watakao tumia njia zisizofaa katika kupata ardhi kubwa pasipo maamuzi ya pamoja
huku akiwataka kutoa ushirikiano kwa wataalam wa ardhi watakaoainisha mipaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) Wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe amewataka wananchi hao kutokubali kurubuniwa na watu watakaojitokeza kudai michango ili waweze kuwapatia ardhi pasipo kufuata utaratibu.
Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Mkoa wa Kigoma, Palmon Rwegoshora amewataka wananchi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu zoezi hilo litakalosaidia kubainisha mipaka.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.