Na Mwandishi Wetu
Wakuu wa idara na vitengo katika Halamshauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameshauriwa kuwasisitiza watumishi walio chini yao kujaza utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwenye mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma (PEPMIS).
Wito huo umetolewa leo Mei 28, 2024 wilayani humo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa halmashauri hiyo, George Msonge alipokuwa anawapitisha baadhi ya watumishi wa Idara ya Elimu Msingi juu ya ujazaji wa majukumu yao katika mfumo huo.
“Idara na vitengo vingine kama zina changamoto ya kutumia mfumo wawasiliane na ofisi ya TEHAMA au ile ya Utawala na Usimaizi wa Rasilimali watu kuona ni namna gani watasaidiwa na tayari watu wa Ukaguzi wa Ndani na Fedha wameomba kupigwa msasa wa matumizi ya mfumo,” amesema.
Naye Afisa Elimu Maalum Msingi wa halamshauri hiyo, Nelistera Kihoza amehimiza watumishi wenzake kuhakikisha wanaujua mfumo huo vyema ili kuwaepusha na matatizo yanayoweza kutokea siku za mbeleni hasa suala la upandaji madaraja.
“Muhimu watu wajitoe kuujua mfumo kwakuwa ni agizo linalopaswa kutekelezwa na haliepukiki ni vizuri kupigana msasa kama hivi naamini changamoto ya kutoufahamu mfumo itakuwa imepatiwa ufumbuzi,” amebainisha.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.