Na Waandishi Wetu
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kudumu kwa Muungano kumetokana na imani na dhamira ya dhati ya waasisi wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na viongozi wengine waliofuata.
Samia amebainisha hayo usiku wa leo alipozungumza na taifa kutoa salamu zake za miaka 60 ya Muungano.
"Zipo nchi nyingi zilijaribu kuungana lakini zilishindwa lakini Muungano wetu umedumu kutokana na udugu na historia iliyotenganishwa na mipaka ya kikoloni lakini kiasili vinasaba (vya pande mbili za Muungano) vinafanana," amesema.
Pia, amebainisha kuwa Muungano umewezesha kwa kiasi kikubwa kulinda Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
"Septemba mwaka huu Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) nalo linatimiza miaka 60 toka kuanzishwa kwake ni wajibu wetu kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ili kulinda mipaka pamoja na watu na mali zao," amesema.
Katika hatua nyingine Samia amebainisha kuwa kutokana na robo tatu ya watanzania kuzaliwa baada ya Muungano nayo ni sababu mojawapo inayosababisha uendelee kudumu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.