Na Mwandishi Wetu
Benki ya CRDB imetoa msaada wa madawati 40 yenye thamani ya shilingi 4,000,000 katika Shule ya Msingi Kabulanzwili iliyomo Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu kutoka faida ya 1% wanayoipata kwa mwaka kuweza kurudisha kwa jamii.
Akiongea baada ya kukabidhiwa madawati hayo leo Jumanne Disemba 3,2024 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu ameishukuru Benki ya CRDB kwa kutoa msaada huo kwakuwa utaboresha miundombinu ya ufundishaji kitu kitakachosaidia watoto kukaa sawasawa na kusoma vizuri.
“Nchi yetu ni kubwa na serikali haiwezi kufanya vitu vyote ndio maana inaweka mahusiano mazuri na wadau tofauti kama hawa CRDB ambao wameona waisaidie serikali kuboresha miundombinu ya elimu baada ya kuona kuna uhitaji wa madawati ndio maana yamekuja hapa,” amesema.
Naye Kaimu Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi, Evodi Kereti amesema wameanzisha program inayoitwa Keti Jifunze inayohusisha kupeleka madawati mashuleni kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji.
“Wito wangu kwenu wanafunzi muyatunze haya madawati napenda nikija baada ya miaka miwili niyakute yapo hivi ili yaweze kutumika na nyinyi hivi sasa na wengine watakaokuja kusoma baadae katika shule hii,” amesema.
Kwa upande wake Afisa Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Elestina Chanafi amebainisha kuwa msaada huo utasaidia kupunguza upungufu wa madawati wa 54% uliokuwepo kabla ya kutolewa hadi kufikia 47%.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.