• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

MKUU WA WILAYA BUHIGWE AFUNGA MAFUNZO YA OPERESHENI MERERANI (JKT) KAMBI YA 825KJ KASULU.

Posted on: May 28th, 2018



Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe  ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia  Jenerali Marco Gaguti akihutubia vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni Mererani (Hawapo pichani) Kambi 825 KJ Mtabila Wilayani Kasulu.(Picha kwa hisani ya mlamamediablogspot.com)

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya Operesheni Mererani waondokane na mawazo ya kuajiriwa bali wajielekeze kwenye kujiajiri kutokana na ujuzi walioupata ili wakawe mfano bora katika jamii. Ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana 798 katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila wilayani Kasulu.

Amsema, mafunzo yasitumike tofauti na malengo kwani jamii inahitaji ulinzi mkubwa kutoka kwa vijana hao kwa kushirkiana na vyombo  vya dola ili kutoa taarifa za uhalifu. Pia amewataka kuepuka vishawishi na kulinda Afya zao kwa kutotumia vilevi, kufanya zinaa na starehe nyingine hatarishi.

“Hongereni sana kwa kutimiza vigezo vinavyotakiwa, mmeonyesha utofauti kwani mmejengeka katika dhana ya JKT ambayo ni  uhodari, uzalendo, utii na uaminifu. Hongereni pia  kwa kazi nzuri mliyoifanya Kilimo kwanza kwa kuimarisha usalama na kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa wakulima” amesema   Gaguti.

Amehitimisha kwa kuahidi kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mh. Yohana Mshita katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Umeme pia kuhamisha Barabara inayopita kambini ili ipite nje ya eneo hilo.

Wakisoma  risala, wahitimu hao wamemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua changamoto ya ukosefu wa Umeme iliyopo kambini hapo pamoja na barabara kupita katikati  ya kambi ya kikosi. Aidha, Wamefanikiwa kujenga nyumba ya Mkuu wa kikosi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha uzalendo wao na bidii. Wameushukuru uongozi wa Serikali ya Rais. John Pombe Magufuli pamoja na kikosi kwa kazi nzuri zinazofanyika.

Hafla hiyo imehitimishwa kwa  utoaji wa zawadi kwa vijana walioonyesha umahiri katika nyanja mbalimbali wakati wa mafunzo kambini hapo.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • PAMBA KUINUA UCHUMI WA WAKULIMA

    May 08, 2025
  • WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAHASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.