Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu,amesema zao la pamba limeleta matumaini mapya kama zao la biashara wilayani humo, tofauti na zamani ambapo wakulima walilima zaidi mazao ya chakula.
Akifunga kikao cha wadau wa pamba leo Alhamisi Mei 8,2025,Kanali Mwakisu amewahimiza wakulima kuendesha vyama vya ushirika kwa kufuata miongozo ya serikali na kushirikiana vizuri na Kiwanda cha NGS ambacho kitakuwa mnunuzi mkubwa wa pamba.
Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma,Richard Majalla, amesema serikali imewekeza matrekta,wataalamu,viatilifu na mbolea za ruzuku ili kuongeza uzalishaji na kupunguza ugumu kwa wakulima.
Mkaguzi wa Pamba wa Wilaya ya Kasulu, Michael Kihiga, amesema kuwa msimu huu watatumia mizani ya kidigitali kuhakikisha uwazi wa vipimo na taarifa kufika kwa wakulima moja kwa moja kupitia simu.
Naye Meneja Uendeshaji NGS,Mabulla William amehaidi kuishauri kampuni yake ili iweze kupanga bei bora na hivyo wakulima kunufaika.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Ndelekwa Vanica amesema watahamasisha wakulima kulima pamba kwani itaongeza mapato ya halmshauri kwa kuchukua 3% ya kila kilo itakayouzwa kiwandani.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.