• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Posted on: April 29th, 2025


 Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Emmanuel Ladislaus, amesema mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya uandikishaji wakati wote wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili, ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi na weledi.

_

Akizungumza leo Jumanne Aprili 29, 2025 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari hilo katika Chuo cha Ualimu Kasulu, Ladislaus ameeleza kuwa ingawa mawakala hao wataruhusiwa kuwa vituoni, hawataruhusiwa kuingilia majukumu ya maafisa waandikishaji.

“Ni muhimu mawakala wawe na mipaka ya utekelezaji wa kazi zao ili kuepusha mwingiliano usio wa lazima na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi,” amesema Ladislaus.


Katika hatua nyingine, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatunza vifaa vyote vitakavyokuwa katika vituo vya uandikishaji na kufuata kwa makini maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwandikishaji.

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wamesema yamewajengea uwezo mkubwa wa kiutendaji. Yasinta Kasunzu amesema mafunzo hayo yatamsaidia kusimamia vyema waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki katika kituo chake.

_

Naye Essau Hinyura ameeleza kuwa mafunzo hayo yameongeza weledi wake katika kusimamia shughuli za uandikishaji, huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi pindi awamu ya pili ya zoezi hilo itakapoanza, ili waweze kupata haki ya kushiriki uchaguzi kama inavyotakiwa na Katiba.

_

Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili linatarajiwa kuanza Mei 1 hadi 7, 2025. Wananchi wote wenye sifa wanahimizwa kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha au kuhakiki taarifa zao.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • PAMBA KUINUA UCHUMI WA WAKULIMA

    May 08, 2025
  • WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAHASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.