Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Ndelekwa Vanica, amewapongeza washiriki wote waliopata fursa ya kushiriki katika mafunzo ya maandalizi ya kazi ya kuandikisha watu katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Awamu ya Pili, akisema ni hatua muhimu na ya msingi kuelekea utekelezaji bora wa majukumu yao.
_
Vanica ametoa pongezi hizo leo, wakati akihitimisha rasmi mafunzo hayo katika Chuo cha Ualimu Kasulu, muda mfupi uliopita.
"Nimefurahishwa sana kuona utayari na moyo wa kujifunza miongoni mwenu. Naamini kuwa kupitia mafunzo haya, mmepata ujuzi na mbinu muhimu zitakazowasaidia kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi," amesema Vanica.
Ameongeza kuwa ana matumaini makubwa kuwa washiriki hao watakuwa mabalozi wazuri wa halmashauri watakapokwenda kutekeleza kazi katika maeneo yao.
"Ninaamini mtawakilisha vema halmashauri yetu kwa nidhamu, uwajibikaji na weledi. Mafanikio yenu ni mafanikio ya halmashauri nzima," amesisitiza.
Aidha, amewataka washiriki hao kufanya kazi kwa bidii na kujituma bila kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
"Sitatarajia kusikia manung’uniko yoyote kutoka maeneo ya kazi. Badala yake, nawaamini kuwa mtakuwa mfano wa kuigwa katika utendaji bora. Mkafanye kazi kwa bidii ili kuleta tija kwa jamii tunayohudumia," amehitimisha.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.