Na Mwandishi Wetu
Shirika lisilo la kiserikali la World Vision leo Alhamisi Julai 18,2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limekabidhi kwa jamii miradi mitatu ya matundu kumi ya vyoo katika Shule ya Msingi Muungano pamoja na madarasa mawili ya kisasa katika shule mbili tofauti za msingi Mvugwe na Nyarugusu.
Ambapo kwa matundu ya vyoo mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 53 huku kwa kila shule moja madarasa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 77.3.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja Miradi wa shirika hilo,Donasian Severine amesema kuwa uwa wanaipa jamii miradi kwanza kuangalia kama kuna mapungufu yaliyojitokeza ili mkandarasi aweze kuyarekebisha kabla ya kukabidhi kwa serikali.
"Kipindi cha miezi mitatu ni cha matazamio kuangalia yale yanayohusiana na mkandarasi ili aweze kurekebisha mfano bati kuvuja au vigae kusogea...lakini vile ambavyo haviendani na mkandarasi mfano mtoto kuvunja kioo au ukwanguaji wa rangi hivyo hatohusika navyo," amesema.
Aidha,amebainisha kuwa shirika hilo liliamua kutekeleza miradi hiyo ili kuweka uwiano wa wanafunzi kwenye madarasa pamoja na kuwakinga na viatarishi vya afya kitu kitakachosaidia ustawi wao kuimarika.
Afisa Elimu Awali na Msingi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Elestina Chanafi amesisitiza suala la utunzaji wa miundombinu hiyo ili ipate kutumika na vizazi vingi.
"Watanzania tuna tabia ya kudharau vitu ambavyo si vya kwetu tujitahidi kuitunza miundombinu hii kwakuwa mtu akikupa kitu ukakitunza unampa moyo wa kukupa kingine," amebainisha.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.