Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwalkisu amewataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji walioshinda uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kuhimiza suala la amani katika maeneo yao ya utawala ili yale waliyokuwa wanayanadi kwa wananchi kipindi cha kampeni waweze kuyatekeleza.
Kanali Mwakisu ametoa rai hiyo jana alipokuwa anafunga mafunzo ya uongozi kwa makundi hayo katika Shule ya Sekondari Bogwe wilayani humo tukio lililoendana na viongozi hao kula viapo vya utii na uadilifu.
“Hongereni sana kwa namna mlivyohubiri amani kipindi cha kampeni na hadi siku ya uchaguzi unafanyika usalama ulikuwa umetamalaki niwatie shime muuendelee na moyo huo kwakuwa usalama ukiyumba hata watu waliowachagua mtashindwa kuwaongoza,” amesema.
Aidha,amebainisha kuwa baada ya kushinda uchaguzi wanapaswa kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi, licha ya kuwa na itikadi tofauti za kisiasa pamoja na kufuata maelekezo ya viongozi wa ngazi ya juu ili waongoze wananchi vizuri.
“Usiwe kiongozi ambaye unagawa watu kwamba hawa ni wakwangu na hawa si wangu huko mbele utafeli katika uongozi,niwaombe mkawe shirikishi mkafanye kazi na watu kwakuwa wao ndio wamewaweka katika nafasi hizo mlizoshika,” amesema Kanali Mwakisu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.