Waziri wa Maji na umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (mwenye miwani) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu Godfrey Mbuza wakati akikagua wa ujenzi wa Tanki la Maji katika kata ya Rungwempya.
Muonekano wa Tanki la Maji lililojengwa katika kijiji cha Kasangezi kata ya Kigembe.Mradi huu ni kati ya miradi iliyokaguliwa na Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa.
Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Wakazi wa Kata ya Rungwempya(hawapo pichani) mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa miundombinu katani hapo.Baadhi ya wakazi wa kata ya Rungwempya waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa alipoongea nao mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya Maji katani hapo.Waziri wa Maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (Mwenye miwani) akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Kasulu pamoja na Mkuu wa wilaya. (Wa kwanza kulia kwake) Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Mh. Daniel Nsazugwanko, (wa kwanza kushoto kwake) ni Ndg. Mbelwa Chidebwe Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kasulu(wa tatu kushoto kwake) ni Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Simon Anange.
Na.Andrew Mlama-Kasulu.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, amewataka Makandarasi na wengine waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji kuwa wazalendo na waaminifu kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo ipasavyo kwa manufaa ya wananchi wote.
Waziri Mbarawa ameyasema hayo leo tarehe 27.11.2018, akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi na utekelezaji wa miundombinu ya maji katika kata za Rungwempya na Kigembe zilizopo wilayani hapa ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Kigoma.
Hyo yamejiri wakati wa akikagua ujenzi wa Tanki la maji katika kata ya Rungwempya ambapo amemuagiza Mkandarsi abomoe na kuijenga upya sehemu ya Tanki hilo amabayo ilikua na nyufa hapo awali kabla ya kulifanyia usafi wa nje uliopelekea kufunikwa kwa nyufa hizo.
“Nakuagiza Mhandisi wa Maji uhakikishe Mkandarasi anafumua sehemu ya Tanki ambayo ilikua na nyufa kisha kuijenga upya na kuweka maji ndani kwa Muda wa siku saba kwa ajili ya kulifanyia majaribio ili kujua iwapo linavuja. Aidha Mhandisi wa maji, nakuagiza uwe unafika mara kwa mara eneo la ujenzi wa Tanki na kuhakikisha Mkandarasi anafanya kazi kwa ufanisi ili mradi ukamilike na kuanza kutumika haraka” amesisitiza Mbarawa.
Akiongea na Wakazi wa kata ya Rungwe mpya, Waziri Mbarawa amesema Serikali haiwezi kuendelea na Wakandarasi wasio na sifa. Iwapo Mkandarasi huyo hatamaliza kazi ndani ya muda uliopangwa atamsitisha na kumfukuza ili asiendelee na kazi. Amewataka wakazi wa Rungwempya kuulinda mradi huo na kuepuka uharibifu wa miundombinu yake.
Akikagua Mradi wa maji katika Kata ya Kigembe, Waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi kwa kushirikiana na Mhandisi wa maji wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa miundombinu maeneo ambayo hayakamilishwa ya mradi huo ndani ya muda mfupi kuanzia sasa.
Mbarawa amemuagiza afisa wa TAKUKURU, kufanya uchunguzi wa eneo la Kilomita Nane ili kupata Thamani halisi ya mabomba yaliyotumika katika ujenzi wa mradi huo wa maji. “Nakuagiza na nnakuamini utatekeleza, hakikisha unafuatilia Thamani halisi ya gharama za mabomba yaliyotumika katika ujenzi wa mradi huu yenye urefu wa Km. Nane na taarifa uiwasilishe kwangu haraka iwezekanavyo” amesisitiza Mbarawa.
Waziri amemuagiza Mkandarasi arekebishe maeneo yote ya mabomba ambayo yanavuja, ahakikishe maji yanafikishwa katika shule ya Sekondari Kasangezi iliyopo katani hapo na aweke bomba la chuma sehemu linapohitajika badala ya kutumia la Plastiki. Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu, kufuatilia mara kwa mara na kuhakikisha maagizo yake yanafanyiwa kazi kuhusiana na miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayaya Kasulu, ndg. Mbelwa Chidebwe, amesema wao kama chama jukumu lao kubwa ni kuhakikisha Ilani ya chama inatekelezwa kwa kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.
“Hatufanyi kazi kwa lengo la kumnyanyasa mtu au kumuonea bali tunahakikisha tunaisimamia Ilani ya Chama chetu kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa Kasulu na Tanzania kwa ujumla” amesema Chidebwe.
Wananchi waliojitokeza kumsikiliza na kujionea ukaguzi huo uliofanywa na Waziri, wamemshukuru kwa kufika mwenyewe katika maeneo yao na kujionea changamoto zinazopelekea huduma hiyo muhimu kutowafikia kwa usahihi kutokana na baadhi ya watendaji kutokua waadilifu na kutotekeleza maelekezo na maagizo ya Seriakali kwa ufasaha.
Waziri Mbarawa amehitimisha ziara yake kwa kukagua miradi ya maji katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu na Wilaya ya Buhigwe.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.