Na Mwandishi Wetu
Serikali imewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kila siku katika mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma (PEPMIS).
Hayo yamebainishwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma na Victoria Panga kutoka Ofisi ya Rais Utumishi kwenye mafunzo yaliyolenga kubaini changamoto zilizojitokeza kwenye utumiaji wa mfumo huo yaliyohusisha wakuu wa idara na vitengo,wakuu wa sehemu,wakuu wa shule za msingi na sekondari,wakuu wa vituo vya afya pamoja na watendaji wa kata katika halamshauri hiyo.
“Nawashukuru kwa ajili ya kushiriki mafunzo haya hili jambo ni la kitaifa na lina maelekezo kwahiyo tuwaombe watumishi muwe ‘serious’ katika hili jambo kwasababu linaenda kugusa maslahi yetu kwahiyo usipotekeleza kuna vitu vitatokea kama kupanda madaraja unaweza kukosa vitu kama hivyo,” amesema.
Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Magdalena Segeja amesema kuwa hivi sasa kila mtumishi atapimwa kupitia mfumo huo hivyo asipofanya jitihada kuhuisha taarifa zake mfumo utamsoma sifuri kwenye utendaji wake wa kazi.
“Nawahasa sana watumishi wenzangu ni maelekezo ya serikali kuhusu huu mfumo kwa sasa hatuna tena ile OPRAS tuliyokuwa tumezoea kuijaza kwa mkono sasa hivi tunapimwa kwenye mfumo kwahiyo mtu akichukulia uzembe asipojaza taarifa zake mfumo utamsoma sifuri,” amebainisha.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.