Afisa Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu ndg. Nicholaus Elihaki akiwasilisha mada wakati wa utoaji wa mafunzo kwa watumishi waajira mpya kada ya watendaji wa vijiji yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Kasulu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Ndg. Nimrod Kiporoza akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya watumishi wa ajira mpya kada ya watendaji yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu. kushoto kwake ni Afisa Utumishi wilaya ya Kasulu ndg. Charles Millinga pamoja na Afisa Tawala (W) Nicholaus Elihaki
Mratibu wa TASAF Halamshauri ya wilaya Kasulu, Almachius Njungani akiwasilisha mada kwenye mafunzo elekezi kwa watumishi wapya kada ya watendaji wa vijiji yaliyofanyika wilayani hapa.
Na. Andrew Mlama-Kasulu.
Watumishi wa ajira mpya kada ya watendaji wa vijiji walioajiriwa kati ya mwaka 2015 hadi 2018, wamepatiwa mafunzo elekezi yatakayowasaidia katika kuboresha utendaji wao wa kazi ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu katika maeneo yao ya utendaji kazi wilayani hapa.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 29/10/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya kasulu, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu ndg. Nimrod Kiporoza amewataka watendaji hao kuzingatia maelekezo yatakayotolewa ili wakayatumie katika kuboresha utendaji kazi wao kwa kuzingatia sheria kanuni na maadili ya kiutumushi.
Amesisitiza kuwa, mafunzo hayo yatumike kukumbushana majukumu ya utendaji yanayohusu maeneo mbalimbali ya utendaji kazi .Aidha amewataka wataalam wa Idara na Vitengo vingine wasaidie kutoa maelekezo na ujuzi kwa watendaji hao utakaosaidia kupanua uelewa wa mambo mengi zaidi ya utendaji kazi.
“Jifunzeni vizuri ili mjue Sheria na Kanuni zinazowaongoza katika utendaji kazi wenu ili msiyumbishwe pale mnaposimamia utekelezaji wa kazi. Ikumbukwe watendaji ndio wasimamizi wa utekelezaji wa kazi na shughuli nyinginezo za maendeleo vijijini”amesema Kiporoza.
Akiwasilisha mada, Afisa Tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu ndg. Nicholaus Elihaki amefafanua kuwa, utumishi wa Umma unategemea nidhamu kubwa kwa watumishi ili kuepuka migogoro na muajiri itakayopelekea kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Amesema watumishi wanapaswa kufikia malengo ya kinidhamu ili kudumisha utumishi wenye weledi. Amesisitiza watumishi waepuke makosa makubwa na madogo ya kuitumishi ili kujiepusha na migogoro dhidi ya muajiri na jamii wanayoihudumia.
‘’Watumishi wa tuhakikishe tunazingatia kanuni za utendaji katika utumishi wa umma, ikiwemo kuzingatia masaa ya kazi, mahudhurio sahihi, kuzingatia kanuni na miongozo ya kazi katika jamii tunazoishi na mazingira tunayofanyia kazi. suala la upandishwaji vyeo, kuthibitishwa kazini pamoja na huduma nyingine za kiutumishi ni jukumu la muajiri kuendana na miongozo iliyowekwa” amehitimisha Afisa Tawala.
Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu, ndg. Charles Millinga, amewasilisha mada kwa kuwafafanulia watumishi hao kuhusu haki na wajibu wa mwajiri pamoja na mtumishi, namna bora ya mawasiliano katika ofisi za Umma,taratibu za mafunzo na kujiendeleza kitaaluma, ujazaji wa OPRAS, kanuni bora za utendaji kazi na nidhamu kwa watumishi wa Umma.
Wakuu wa idara na vitengo vya manunuzi na ugavi, fedha, kilimo, utumishi na utawala, sheria, uchaguzi, ardhi na maliasili, maendeleo ya jamii pamoja na TASAF walipata fursa ya kuwasilisha mada zao na kutoa maelekezo ya kiutendaji kwa watumishi hao ili kuwajengea uwezo, uelewa na ufahamu wa utekelezaji majukumu yao kwa mujibu wa sheria na miongozo ya seriakali.
Kwa upande wao, watendaji wameonyesha kufurahishwa na mafunzo hayo na kuiomba Idara ya utumishi na utawala na halmashauri kwa ujumla, kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili kuwajengea weledi na uelewa wa masuala mbalimbali ya utendaji kazi. “Mafunzo haya yamepelekea kujijengea uwezo katika utendaji kazi kwa kutupa ufahamu wa kutatua changamoto mbalimbali. Aidha yametuwezesha kufahamu sheria kanuni na taratibu za kazi ambazo hapo awali hatukuwa na ufahamu nazo” alihitimisha Emiliano Fabiano, afisa Mtendaji wa kijiji cha Mgombe kata ya Nyakitonto wilayani hapa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.