Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Dkt. Semistatus H. Mashimba leo Ijumaa Februari 7,2025 amefanya kikao na watendaji wa sekta ya afya katika Ukumbi wa Kagoma uliopo makao makuu ya halmashauri.
Ambapo kupitia kikao hicho amewataka watendaji hao kufuata sheria na taratibu za afya zilizopo,kutoa elimu kwa jamii kuepeukana na magonjwa ya mlipuko pamoja na kukatia risiti ya kieletroniki makusanyo wanayoyafanya ili yasome kwenye mfumo.
Aidha,Dkt.Mashimba ameelekeza usimamizi mzuri wa mapato ili kuongeza makusanyo ya halmashauri pamoja na vifaa tiba vinavyoletwa katika vituo vyao kama njia mojawapo ya kuboresha huduma za kitabibu kwa wananchi.
Kikao hicho kilihusisha washiriki kutoka Timu ya Usimamizi wa Afya ya Halmashauri (CHMT),waganga wafawidhi,wahasibu na wafamasia wa vituo vya kutolea huduma za afya.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.