Na Mwandishi Wetu
Wanawake mkoani Kigoma wametakiwa kuchangamkia fursa kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji kwa kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili watoe mchango wao katika vyombo hivyo muhimu vya maamuzi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania Mkoa wa Kigoma, Agripina Buyogera hivi karibuni kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yalifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
“Afisa Maendeleo ya Jamii utusaidie kuandaa wamama kule kwenye vikundi kama mtu ameshakuwa kiongozi huko na anasimamia pesa vizuri anashindwaje kuongoza kijiji, mtaa au kitongoji kwahiyo wagombea tunao msiogope hakikisheni mnasimama imara,” amesema.
Aidha, ameitaka serikali kuhakikisha inaboresha upatikanaji wa mikopo kwa wakinamama kwakuwa iliyopo sasa haiwatoshelezi katika kuendesha shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma, Josephine Genzabuke amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kielelezo cha wanawake wa Tanzania walivyo shupavu kutokana na uongozi wake kufanya mambo mengi makubwa hasa katika Mkoa wa Kigoma.
“Kazi kubwa amefanya Mama Samia tumeshuhudia barabara zikiendelea kujengwa, vituo vya afya vinajengwa na hospitali kukarabatiwa ikiwemo ile ya Mkoa wa Kigoma ambayo kwa sasa wananchi hawateseki kwenda Bugando au Muhimbili kwakuwa mahitaji yote yanapatikana pale,” amesema.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.