Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),Mary Chatanda amewahamasisha wanawake wilayani Kasulu kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ili kuchochea maendeleo hapa nchini.
Mary ametoa wito huo jana Julai 15,2024 wilayani humo alipofanya mkutano wa adhara kuzungumza na wanachi wananchi wakati wa ziara ya viongozi wa UWT Taifa mkoani Kigoma.
Amesema uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyia baadae mwaka huu wanawake wajitokeze kuomba na kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa uwezo mkubwa aliouonyesha Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye masuala ya uongozi umeakisi ni namna gani wanawake wanaweza kuongoza.
Aidha,amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanaboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura zoezi linarotarajiwa kuanza Julai 20,2024 mkoani Kigoma kwa kufika katika vituo vilivyopangwa.
“Kubwa tunalopita kuhamasisha kuanzia tarehe 20 tukaboreshe taarifa zetu kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura wale wenye vichinjio na wamehama eneo moja kwenda eneo jingine inawezekana ulikuwa unakaa kijijini ukahamia mjini nenda na kadi yako ya mpiga kura ili taarifa zako ziboreshwe,” amesema.
Tofauti na hayo pia amehimiza utunzaji wa mazingira kwa kuwataka wakazi wa wilaya hiyo kuepuka matumizi ya nishati chafu, ukataji wa miti pamoja na utupaji taka ovyo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.