Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Mhe. Agustino Vuma Holle jana Machi 17,2025 amefuturisha wananchi wa Wilaya ya Kasulu ikiwa ni sehemu ya kila mwaka kufanya hivyo kipindi cha mfungo.
Ambapo kupitia hafla hiyo amesema kuwa tangu Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani katika jimbo hilo ameongeza fedha za maendeleo zilizosaidia kupasua barabara nyingi maeneo ya vijijini kitu kilichosaidia mawasiliano kuimarika.
Aidha, Vuma amewaelekeza wataalam wote waliodhuria tukio hilo kuyachukua mawazo yote ya wawakilishi waliotoka katika kila kata jimboni humo na kuyafanya kuwa mpango kazi wao kwenye utendaji kwakuwa wamefikisha sauti za wananchi.
Naye Kamishna wa Uhifadhi wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),Prof. Dos Santos Silayo amebainisha kuwa baada ya miaka 12 misitu wanayoisimamia wilayani humo itaanza kuvuna magogo kitu kitakachowavutia wafanyabiashara wengi kuja hivyo uchumi kuimarika.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu pamoja na kuwa na eneo kubwa la kiutawala lakini wanajitahidi kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati.
Katika hatua nyingine kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,Ndelekwa Vanica amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo imekuwa na ufanisi mkubwa kutokana na Mhe. Vuma kuishi na watumishi vizuri kwa kutoa maelekezo kwa kufuata sheria,miongozo na taratibu za nchi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.