Na Mwandishi Wetu
Timu ya maafisa elimu msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imefanya ufuatiliaji kwa walimu waliopata mafunzo ya ufundishaji wa somo la kiingereza kupitia Mradi wa Shule Bora katika shule za msingi za Nyakitonto na Murubanga.
Akizungumza leo katika Shule ya Msingi ya Nyakintonto Afisa Elimu Taaluma (Msingi) wa Halmashauri hiyo,Joseph Maiga amesema kuwa ufuatiliaji huo umelenga kuona namna gani waliopatiwa mafunzo walivyoweza kufikisha kwa walimu wenzao pamoja na kuboresha ufundishaji kwa wanafunzi.
Aidha, Maiga amesema kuwa lengo la Mradi wa Shule Bora ni kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya ufundishaji pamoja na kuimarisha usimamizi wa shule na kwa mwaka huu tayari umeendesha mafunzo kwa walimu wakuu 88 wa shule za msingi na maafisa elimu kata 21 juu ya uanzishwaji wa jumuiya za kujifunza (JZK).
Naye Mwezeshaji wa Somo la Kiingereza katika halmashauri hiyo,Mary Mollel,amesema kuwa hadi sasa wameweza kuwawezesha walimu wote wa darasa la kwanza na pili katika Kata ya Nyakitonto na siku zinavyokwenda mbinu wanazowawezesha wanaendelea kuzitumia darasani.
Katika hatua nyingine mwalimu aliyepata mafunzo ya JZK, Gaudence Barakenyanya amesema kuwa baada ya kutoka katika mafunzo hayo walipita katika baadhi ya shule kuwafundisha mbinu bora za kufundisha somo la kiingereza na juu ya kuandaa vipindi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.