Na Mwandishi Wetu
Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ikiongozwa na Kaminshna wa tume hiyo, Amina Talib Ali jana Jumanne Juni 11,2024 imetoa elimu kwa umma kuhusiana na misingi ya utawala bora na haki za binadamu kwa baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Akizungumza katika tukio hilo Amina amesema kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwakumbusha watendaji hao ni namna gani wanaweza kutekeleza majukumu yao kwa kufuata haki za binadamu pamoja na misingi ya utawala bora.
“Tofauti na watendaji lakini pia tutafanya mikutano ya adhara na wananchi waelewe majukumu yetu ili haki zao zinapovunjwa waelewe malalamiko yao wanayapeleka wapi ili yaweze kushughulikiwa, kwakuwa THBUB ipo kikatiba na inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria,” amesema.
Naye Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma Mawasiliano Utafiti na Nyaraka wa tume hiyo, Joshua Taramo amesema kuwa dhana ya utawala bora ni zoezi la watu wenye mamlaka na madaraka kutoa maamuzi ya namana gani rasilimali za taifa zitumike katika kuboresha maisha ya wananchi.
“Dhana ya utawala bora inahusu viongozi unapokataa kutoa taarifa ya mapato namatumizi kwa wananchi unakiuka misingi ya uatawala bora…misingi ya utawala bora inajumuisha uwazi,uwajibikaji,utawala wa sheria,usawa, uadilifu,ufanisi na tija,maidhiano,ushirikishaji na mwisho ni mwitikio,” amesema.
Akitoa salamu za shukrani Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Ndelekwa Vanica amesema kuwa ujio wa ugeni huo utasaidia wananchi kutambua haki zao zinapatikana vipi kwenye ofisi za serikali kwakuwa kutakuwa na wigo mpana wa kuuliza maswali.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.