Katika kuendelea kukuza vipaji mashuleni Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa mipira 80 ya miguu katika shule mbili za msingi Kisuma na Kakirungu zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa ya Buyonga, Paul Ramadhani kwa niaba Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele, alipokuwa anasoma hotuba yake siku ya leo Ijumaa Agosti 09, 2024 katika Shule ya Msingi Kisuma.
Ramadhani amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanatia bidii kwenye masomo yao huku wakizingatia michezo kitu kinachoweza kuwafungulia fursa ya ajira ndani na nje ya nchi.
“Soma kwa bidii huku unapiga mpira sababu kupitia michezo unaweza kufikia ndoto zako kwa kuweka bidii kwenye mpira, kwani katika karne hii mpira ni ajira ndio maana serikali imeliona kundi hili na kuligusa”, amesema.
Aidha, ametoa shukrani kwa serikali pamoja na TFF kwa kutoa mipira hiyo katika shule zilizopo Halmashauri hiyo kwani inaonyesha dhamira ya serikali ya kuinua vipaji inatekelezwa.
Kwa upande wake Afisa Elimu Vielelezo Msingi wa halmashauri hiyo, Respice Swetu amewataka walimu pamoja na wanafunzi kuitunza mipira hiyo kama njia mojawapo ya kuienzi michezo katika shule hizo.
Vilevile, ameeleza kuwa shule hizo zimepewa kipaumbele kutokana muhamko walioonyesha kwenye michezo kitu kilichopelekea Shule ya Msingi Kisuma kuwa eneo la michezo kwa shule za msingi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.