Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Mhe Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi kujiandaa kwa ajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaopita katika eneo hilo kuelekea nchini Burundi.
Ambapo amesema mradi huo utajenga stesheni mbili za abiria na mizigo ,ambazo zitaongeza ajira hasa kwa vijana pamoja na kuchangia maendeleo ya uchumi katika wilaya hiyo.
Kanali Mwakisu ameyabainisha hayo jana wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kasulu iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Kasulu Mji.
Pamoja na hayo,ameitaka jamii kujikinga na ugonjwa wa MPOX akitolea mfano hatua zilizochululiwa wakati wa UVIKO-19 hivyo wachukue tahadhari ili kulinda afya zao.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Mbelwa Chidebwe, amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kuwaasa kutotumika kama madaraja ya kuwachafua wengine kitakapofika kipindi cha uchaguzi.
Naye Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Masoud Kikoba amewahimiza vijana kulinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwakuwa inatumia gharama nyingi kwenye utekelezaji wake hivyo ni jukumu lao kuhakikisha inakuwa salama.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.