Na. Andrew Mlama-Kasulu.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Mstaafu Emmanuel Maganga, amewaagiza wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Kilimo wa Halmashauri za Buhigwe, Kasulu na Kasulu mji, kuhakikisha mbolea inapatikana na kusambazwa kwa wakulima kabla ya msimu wa kilimo kufikia mwisho hata kwa kutumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania itakapobidi.
Hayo ameyasema leo Tarehe 16.11.2018, alipokua katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa kukutana na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo mkoani hapa.
“Mtakapo shindwa kupata namna bora ya kusafirisha mbolea wasilianeni nami ili niagize Jeshi la Wananchi wa Tanzania, ili waweze kuwasaidia kusafirisha mbolea hiyo na kuwafikia wananchi kabla ya msimu sahihi wa matumizi ya mbolea kufikia tamamti” amesisitiza Maganga.
Maganga amewataka maafisa Kilimo watekeleze majukumu yao kwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya Mbegu bora, badala ya kurudia kupanda zile walizozivuna ili kuhakikisha wanapata mazao mengi zaidi.
Maganga amehitimisha kikao chake na viongozi hao, kwa kuwataka kusimamaia maelekezo ya Serikali kuhusu kuzuia vifo vya wazazi na watoto kwa kuhakikisha akina mama wanajifungua mahali salama. Aidha amewakumbusha kusimamaia masuala ya lishe na kukabiliana na Changamoto ya ugonjwa wa Malaria.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.