• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe ya Ofisi |
Kasulu District Council
Kasulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo-Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
      • MRADI WA UMWAGILIAJI TITYE
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogondogo
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Taratibu
    • Huduma Kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Makala
    • Matangazo

"KUWENI WAADILIFU NA MSIMAMIE MAAZIMIO KULINDA RASILIMALI ZA WILAYA"-RC MAGANGA

Posted on: September 16th, 2019

Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Wataalam pamoja na waalikwa wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Kagerankanda Mhe. Ezekiel Mshingo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kitalu cha uwindishaji wa Kkitalii cha Makere-Uvinza Open Area kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma(Hayupo pichani)

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu. Emmanuel Maganga akisisitiza jambo  mara baada ya kupokea taarifa ya Eneo la kitalu cha uwindishaji wa kitalii cha Makere-Uvinza Open Area Kasulu.

Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Madiwani, Wataalam pamoja na waalikwa wakisilkiliza maelekezo na ushauri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu leo Tarehe 16.09.2019

Na. Andrerw Ginnethon-Kasulu.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia  Jenerali  Mstaafu Emmanuel Maganga, amefanya kikao kazi na Braza la Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu na kusisitiza utendaji kazi unaozingatia uadilifu na kusimamia utekelezaji wa maazimio wanayokubaliana kwenye vikao vya kisheria ili kuepuka migogoro inayopelekea kushindwa kusimamia kitalu cha uwindishaji kilichopo wilayani hapa.

Magaga ameyasema hayo leo tarehe 16,9,2019 baada ya kupokea taarifa ya Eneo la Kitalu cha uwindishaji wa kitaalii cha Makere Fr-Uvinza Open Area kisha kujadili changamoto zinazotokana na shughuli mbalimbali za kibinaadamu ambazo haziendani na uhifadhi wa wanyamapori na matakwa ya Ardhi Oevu zinazoathiri kitalu hicho.

Akipokea mawazo na ushauri kutoka kwa Wah. Madiwani kuhusu kukabiliana na changamoto hizo, Mkuu wa Mkoa amewaasa kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni na Sheria wakilenga maslahi ya Nchi.

“Utendaji kazi wenye uadilifu na uaminifu pia kusimamia kile tunachokubaliana kwenye vikao, utaepusha migogoro isiyo ya lazima inayosababishwa na uwepo wa maamuzi tofauti kwa baadhi yenu  hali itakayopelekea kutofikiwa kwa malengo katika mipango ya Halmashauri”  Amesisitiza Maganga.

Akitoa taarifa fupi  ya Kitalu hicho,  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kan. Simon Anange,  amesema Wah. Madiwani wahakikishe wanawasaidia wataalam katika kusimamia utekelezaji wa maazimio wanayopanga ili kuepuka mikwamo ya kiutendaji katika usimamizi na uendelezaji wa Kitalu.

“Madiwani simamieni kwa ukamilifu utekelezaji wa maazimio yenu ikiwemo ulinzi na uendelezaji wa Kitalu chetu na tushirikiane kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa manufaa ya Halmashauri ya Kasulu na siyo kundi la watu au mtu binafsi” amesisistiza Kan. Anange.

Akisoma taarifa ya Eneo la kitalu cha uwindaji wa kitalii, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Mwaka 1996 Wizara ya Maliasili na Utalii iliridhia ombi kuhusu  kutambua rasmi eneo wazi lenye ukubwa wa Kilomita za mraba elfu mbili miatano tisini na moja  kuwa kitalu cha uwindishaji kwa jina la Makere Forest Reserve/Uvinza Open Area.

Kupitia taarifa hiyo, Mkurugenzi amefafanua kuwa lengo la Halmashauri katika uidhinishaji wa kitalu hicho ni uhifadhi wa bioanuai, Ardhi oevu katika Mto Malagarasi, wanyama pori, misitu na Kuongeza mapato ya Halmashauri.

Aidha Kasekenya amefafanua kuwa, mpaka sasa kitalu hicho kipo chini ya Kampuni ya Wengert Windrose Safari Ltd inayoendesha shughuli za uwindaji wa kitalii na uhifadhi.  Kampuni hiyo imeweka miundombinu mbalimbali ikiwemo uwanja wa ndege, Barabara, Kambi zenye mahema, mnara wa mawasiliano pamoja na boti kwa ajili ya watalii na ufanyaji wa Doria.

Amezitaja  changamoto zinazokabili eneo la kitalu ikiwa ni ongezeko la shughuli za kibinaadamu kama makazi, kilimo, ufugaji , uwindaji haramu (ujangili), na ugawaji holela wa Ardhi unaofanywa na kundi la wananchi wasiotii Sheria na kuzingatia kanuni na taratibu za Nchi.

Kasekenya amehitimisha kwa kufafanua kuwa, pamoja na uwepo wa changamoto hizo ni muhimu kitalu kiendelee kulindwa kwa kuwaondoa wavamizi na wananchi wengine waliofanya makazi katika eneo la Ardhi oevu.

‘’Mwekezaji anashindwa kuwekeza kwa nguvu kutokana ukosefu wa usalama  eneo la kitalu na uvamizi unaoendelea kwa baadhi ya wavamizi kuua wanyama kwa kutumia sumu, kuingiza mbwa katika hifadhi na mifugo inayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira” amehitimisha  Kasekenya.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO ILIYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 08, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI February 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA February 21, 2024
  • MWALIKO WA ZABUNI KUPANGISHA ENEO KWAAJILI YA MGAHAWA March 08, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • PAMBA KUINUA UCHUMI WA WAKULIMA

    May 08, 2025
  • WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAHASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • MAWAKALA WA VYAMA KURUHUSIWA KITUONI KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

    April 29, 2025
  • Angalia Zote

Video

NAIBU WAZIRI OR-UTUMISHI NOV 2022
Video zaidi

KURASA ZA KARIBU

  • PlanRep_Web_Based
  • FFARS Online Manual
  • PlanRep Online Manual
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • safari_Live
  • safaridemo
  • Dashibodi ya Ukusanyaji wa Mapato
  • UNICEF Dashboard
  • Kamusi Eng & Swa

TOVUTI ZINAZOHUSIANA

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • TAMISEMI
  • BUNGE
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • ARIDHI
  • OPEN UNIVERSITY
  • PSPTB
  • AJIRA
  • HFR Dashboard
  • KIGOMA DC
  • NACTE
  • NECTA
  • eMrejesho

Kihesabu watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

    Anuani ya Posta: S.L.P 97

    Simu ya Mezani: +255-028-2810339

    Simu: +255-028-2810339

    Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera Ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Wasiliana Nasi

Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.