Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezitaka Halmashauri kutumia vyombo vya habari vilivyo karibu na maeneo yao kuwapa wananchi taarifa sahihii za serikali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili wawe na uelewa nazo.
Rais Samia ametoa wito huo leo Juni 18,2024 wakati akifungua Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
"Watu wetu (vijiji) wapewe taarifa kwakuwa watu wa mjini wanakuwa 'not interested'...lakini wenyewe wakisikia eeeh bwana tumejengewa Kituo cha Afya kipya watakuwa na hamu ya kufanya safari kwenda kuona kile kilichotajwa kipo naomba sambazeni hizo taarifa," amesema.
Aidha,amehimiza waandishi wa habari kujikita kwenye kufanya habari za uchambuzi ili kupunguza wingi wa utata wa habari zinazotolewa hapa nchini.
"Kuna uchache wa 'analyst' wa habari taarifa zetu hazifanyiwi uchambuzi mtu anaichukua habari nzima na kuimwaga hivyo hivyo ukiisoma unajiuliza huyu mwandishi wa habari kweli hivi alijiuliza kabla ya kuandika," amesema.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.