Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa ndoto za Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona inafika siku halmashuri zote nchini zinasimama na kuendesha shughuli za kuwaletea wananchi maendeleo pasipo kusubiria ruzuku kutoka serikali kuu.
Mkuu wa Mko wa Kigoma, Thobias Andengenye amebainisha hayo juzi kwenye kikao kilicholenga kufanya tathimini ya vipaumbele vya bajeti katika halmshauri nane za mkoa huo.
Kikao kilichojumuisha uongozi wa ngazi ya juu ya mkoa huo, wakurugenzi na wakuu wa idara na vitengo ili kuangalia ushirikishwaji wa wananchi na kama zinaakisi matakwa yao katika kuwaletea maendeleo.
Amesema katika mchakato wa bajeti unaoendelea ni lazima liwepo hakikisho la vyanzo vya mapato vilivyobuniwa viweze kukusanya vizuri pamoja na kuzuia mianya ya uvujaji wake.
“Tunaweza kukusanya sana lakini wananchi wangependa kuona kile tulichokusanya kutoka kwao kinawasaidia…ukitumia 40% ya mapato ya ndani kujenga zahanati, madarasa, barabara na hata daraja ambalo limekuwa linawasumbua watu kuvuka itakusaidia kutotumia nguvu kubwa kuelezea namna ulivyotumia mapato yako ya ndani,” amesema.
Aidha, Andengenye ameitaka Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu kuhakikisha inahamia katika jengo lao jipya la kiutawala ili kuboresha huduma mbalimbali za kiutendaji kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Joseph Kashushura amesema kuwa kikao hiko kimesaidia kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na menejimenti za halmshauri zingine kitu kitakachoboresha utendaji kazi.
“Uzoefu tuliuoupata kwa njia ya majadiliano kama tutaenda kuufanyia kazi katika maeneo yetu utakuwa msaada mkubwa katika kuboresha shughuli mbalimbali katika maeneo yetu ya kazi,” amebainisha.
Pia, ametoa hakikisho ya kutekeleza maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa likiwemo la kuhamia katika jengo lao jipya la kiutawala.
“Tumejenga jengo jipya katika halmshauri yetu na sasa tunategemea kuhamia kabla ya mwezi wa tatu kwahiyo agizo hilo tutalitekeleza kama ilivyo ili kuendana na maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa,”amebainisha.
Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa huo, Albert Msovela ameto rai kwa wakurugenzi na wahandisi kufanya tathimini ya fedha zinazotolewa katika ujenzi ni namna gani zinaweza kukidhi matakwa ya utekelezaji wa miradi.
Halmshauri zilizoshiriki kikao hicho ni Kigoma, Kasulu Vijijini, Kasulu Mji,Kibondo,Kakonko, Buhigwe pamoja na Uvinza.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.