Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imepongezwa kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba nne za tatu kwa moja kwa watumishi wa kada ya afya uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 460 kupitia mapato ya ndani.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa,Godfrey Mnzava ametoa pongezi hizo leo alipokuwa anafungua nyumba hizo zilizopo eneo la Hospitali ya Wilaya hiyo Nyamnyusi.
“Mhe Mkuu wa Wilaya wengine wanakusanya mapato ya ndani wanaenda kukaa vikao, semina na safari lakini hapa milioni 460 zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi hapa ukiona nyumba moja ni milioni 115 ambayo ina familia tatu,” amesema.
Aidha, Mnzava amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmsahauri hiyo, Dkt. Semistatus H. Mashimba kwa maamuzi mazuri aliyoyafanya yatakayokwenda kutengeneza mazingira rafiki kwa watanzania katika sekta hiyo nyeti ya afya.
“Watumishi watakuwa 'comfortable' kuwahudumia watanzania katika sekta nyeti ya afya ambayo Mhe. Rais baada ya kujenga miundombinu rafiki ya kutolea huduma za afya anaowategemea kutoa huduma kwa niaba yake ni watumishi wa sekta ya afya kwahiyo hapa wamejengewa makazi wakae karibu hata ikitokea dharula watoa huduma inakuwa rahisi kupatikana,” amebainisha.
Kupitia mbio hizo miradi yote 10 iliyokaguliwa ilipokelewa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.