Ilikuwa ni jioni ya Agosti 12, 2020 wakati wa makabidhiano ya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya aliyemkabidhi Mkurugenzi mpya Ndugu Joseph Kashushura. Akiongea wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi aliyemaliza muda wake alitaja baadhi ya mafanikio katika kipindi chake kuwa ni pamoja na ongezeko la mapato ya Halmashauri na kupata hati safi mfululizo, ongezeko la shule za msingi na sekondari, ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya na shamba la Kilimo Kwanza ambalo limechangia kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.