Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imefanya mapitio ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa pamoja na Hospitali ya Shunga Misheni iliyopo Kata ya Buhoro kwa lengo la kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi kwa gharama nafuu.
Akizungumza katika tukio hilo hospitalini hapo jana Februari 1,2025 Makamu Mwenyekiti wa Hlmashauri Hiyo,Raulent Poteza amesema ukamilishaji wa mkataba huo utaenda kuleta unafuu na kusogeza karibu huduma za kitabibu kwa wananchi wa eneo hilo na kata za jirani.
“Sisi tumekuja kwa niaba ya wananchi ukiangalia maudhui ya mkataba utapunguza gharama kwa wananchi linapokuja suala la matibabu…kutoka 150,00 kuja 75,000 kwa kwa yale makundi maalum yanayojumuisha wakinamama,watoto,wazee na wale wanaotoka kaya maskini na sisi kama wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii tunasubiri mchakato unaofuata uchakatwe,” amesema.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Ndelekwa Vanica amesema kuwa kutokana na Hospitali ya Wilaya kuwa mbali na baadhi ya maeneo itasaidia wananchi kuja kwenye hospitali hiyo kupata huduma zinazoakisi na zile zinazotolewa na hospitali yetu kwa gharama nafuu.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Shunga,Henry Ndege amesema kuwa mkataba huo utagusa makundi hayo maalum yatakayopata huduma za afya kwa gharama ndogo kwasababu za kiuchumi kwakuwa yakiachwa kutakuwa na changamoto za kiafya kwa makundi husika.
Awali akizungumza katika tukio hilo Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Tubeti Chacha amesema kuwa Mkataba utaakisi utoaji wa matibabu kwa gharama pungufu ya 50% kupitia viwango vilivyoainishwa katika Bima ya Taifa ya Afya.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.