Na Mwandishi Wetu, Kasulu
Viongozi mbalimbali kutoka makundi tofauti katika jamii wametakiwa kutumia nafasi zao kuhakikisha wanahamasisha wananchi juu ya ujenzi wa vyoo bora na matumizi yake pamoja na suala la kunawa mikono kama njia mojawapo ya kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Kwakuwa kampeni ya ujenzi wa vyoo bora na unawaji mikono si tu hamasa yake ipo kwenye ngazi ya halmshauri lakini hata serikali imekuwa inasisitiza jambo hilo kila siku kama njia mojawapo ya kuhakikisha jamii inakuwa na afya bora.
Wito huo umetolewa leo Jumanne Januari 14,2024 na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Paulo Ramadhani kwenye uzinduzi wa ujenzi wa vyoo bora na unawaji mikono ngazi ya jamii (kaya) na taasisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
“Programu hii tuitilie maanani sisi kama viongozi tunaowakilisha wananchi kuhakikisha tunatoa hamasa kwa jamii juu ya matumizi ya vyoo bora kwasababu linagusa afya zetu tukifanya hivyo haya magonjwa ya milipuko na kuharisha yatakuwa historia kwakuwa watu wataelimika kuzingatia kanuni za usafi,” amesisistiza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mhe. Eliya Kagoma amesema kuwa atahakikisha kupitia vikao mbalimbali vya kamati za halmshauri kuwataka wajumbe wake kwenda kutoa hamasa ya jambo hilo ili jamii iwe na uelewa wa kutosha juu ya faida za ujenzi wa vyoo bora pamoja na suala zima la unawaji mikono.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Tubert Chacha amebainisha kuwa ni wajibu wa kila kaya kuhakikisha inajenga choo bora kwa usahihi na kunawa mikono kila wanapotoka chooni kama njia mojawapo ya kujikinga na magonjwa ya milipuko.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.