Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imetambua mchango wa makarani na wasimamizi wa maudhui walioshiriki sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kuwatunuku vyeti vya ushiriki.
Hayo yamebainishwa na aliyekuwa mratibu wa zoezi hilo wilayani humo, Fadhil Hussein Juma alipozungumza na mwandishi wetu mapema siku ya leo.
Amesema vyeti vipatavyo 1374 vitagaiwa kwa washiriki hao kama njia mojawapo ya kutambua mchango wao wa kusimamia vizuri zoezi hilo.
Na kuongeza kuwa tayari wameshaanza kupita katika kata mbalimbali kuwapatia vyeti hivyo viongozi wa maeneo husika ili viweze kuwafikia washiriki.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.