Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (NSV) siku ya jana Ijumaa Novemba 8,2024 imezindua Kituo cha Majiko Sanifu katika Kata ya Nyakitonto.
Kama njia mojawapo ya kupunguza utumiaji wa nishati chafu za kuni na mkaa ili kukabiliana uharibifu wa mazingira kwa kutumia Majiko Matawi.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Diwani wa Kata hiyo, Daniel Mzababa amesema kuwa faida kubwa ya utumiaji wa majiko hayo ni kutumia matawi badala ya kuni na mkaa kidogo kitu kitakachopelekea ukataji miti kiholela kupungua.
“Kata hii ya Nyakitonto ni kubwa na ina athari kubwa kwenye ukataji wa miti hivyo tukitumia majiko haya sanifu maana yake tumeokoa vizazi vya sasa na vile vinavyokuja kwakuwa ukataji miti ovyo utapungua,” amesema.
Kwa upande wake Mratibu wa Programu ya Mabadiliko ya Tabia SNV,Rozalia Mushi amesema kuwa lengo lao ni kuzihamisha familia kutoka kutumia mafiga matatu na likifanikiwa elimu itatolewa zaidi ya matumizi ya nishati safi ya gesi na umeme ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
Naye Afisa Misitu na Ufuatiliaji wa Matumizi ya Nishati Safi wa Mradi huo, Hassani Omari amebainisha kuwa kuanzia mwaka 2024 hadi 2034 serikali ina mpango kabambe wa kuondoa nishati taka hivyo kupitia matumizi ya majiko hayo anaona kufanikiwa kwake.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.