Na Mwandishi Wetu
Serikali imetoa mrejesho wa utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango lililotaka uchimbwaji wa kisima kufanyika mara moja ili wananchi wa Kata ya Nyakitonto waondokane na changamoto ya upungufu wa huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya matumizi yao majumbani.
Akizungumzia utekelezaji wa agizo hilo siku ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Dkt. Semistatus H. Mashimba ameupongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo kwa namna walivyotekeleza agizo hilo kwa wakati ili kusogeza karibu huduma hiyo muhimu kwa wananchi.
Na kuongeza kuwa hatua ya kwanza ya uchimbaji wa kisima tayari imeshakamilika na utekelezaji wa hatua ya pili unasubiri fedha kutoka serikali kuu ili uwekwaji wa miundombinu uweze kufanyika.
“Tuliona ni busara kuwaeleza agizo namba moja tayari limeshatekelezwa kwamba kisima kimeshachimbwa lakini lingine kwasababu tunatekeleza miradi hii kwa hatua sasa hivi tunasubiri fedha kutoka serikali kuu zije kuweka miundombinu kuhakikisha tunafikisha maji kwa wananchi,” amesema.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kasulu,Edward Kisalu amesema kuwa baada ya uchimbaji wa kisima hatua inayofuta itakuwa ni kuweka pampu ya kuvuta maji, na kufunga mabomba ili maji yaweze kuelekea kwenye tangi.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata hiyo, Daniel Maforo amempongeza Mkurugenzi kwa utekelezaji wa ilani ya chama hicho pamoja na moyo wake wa kujitoa mara kwa mara wa kuja kusikiliza kero mbalimbali za wananchi katika eneo hilo.
Mmoja wa wananchi waliodhuria tukio hilo, Tegemeo Raulenti amewaasa wakazi wa kata hiyo kuwa wavumilivu mchakato huo unapoendelea kwakuwa uwekaji wa miundombinu ya maji wa RUWASA ni tofauti na ile waliyoizoea ya serikali za vijiji kwakuwa inalenga kuhudumia idadi kubwa ya watu.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.