Wakurugenzi wa halmashauri nchini wametakiwa kujifunza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma iliyotekeleza ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya wa Hospitali ya Wilaya hiyo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 800 kupitia mapato yake ya ndani zenye uwezo wa kuchukua kaya 17.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk Mfaume Rashid ameyabainisha hayo wilayani humo hivi karibuni kwenye majumuisho ya ziara ya timu ya wataalamu wa ustawi wa jamii na lishe kutoka halmashauri zote za mkoa huo.
Ambapo amempongeza aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Joseph Kashushura aliyehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kwa ubunifu huo uliowasaidia watumishi hao kukaa karibu na vituo vyao vya kazi.
“Wote tunafahamu ugumu wa mazingira kama Kigoma, Katavi na sehemu zingine halmshauri inapokuwa na mfumo mzuri wa makazi bora kwa watumishi wa afya kwa ujenzi mzuri wa nyumba za watumishi kwa kiwango kile cha Kasulu DC kwa zaidi ya watumishi 17 na familia zao tena katika mazingira ya hospitali kwakweli inatia moyo sana,” amebainisha.
Aidha, amemtaka Katibu Tawala wa mkoa huo,Albert Msovela kutoa cheti cha pongezi kwa mkurugenzi huyo kwa kazi kubwa aliyoifanya kupitia ujenzi huo.
Credit: ortamisemi
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.