Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imehitimisha shughuli ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo Ijumaa Novemba 28,2024 katika Shule ya Sekondari ya Bogwe.
Huku vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo vimeonesha kuridhishwa na kupongeza mchakato mzima wa zoezi hilo kwa namna lililovyoendeshwa wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha zoezi hilo Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo,Dkt. Semistatus H. Mashimba amewata wenyeviti wa vijiji na vitongoji walioshinda kutambua kuwa uchaguzi umekwisha na hivi sasa watu wanatakiwa kurudi katika shughuli zao za kawaida ikiwemo kuvunja makundi yote yaliyotokeza.
Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia shughuli za kuwahudumia wananchi kwenda vizuri na itakuwa njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.