Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma inatarajiwa kuwa mwenyeji kimkoa wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Victoria Makyao ameyabainisha hayo leo wilayani humo alipozungumza na mwandishi wetu muda mfupi uliopita.
Amesema maandalizi yote kwa ajili ya kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo tayari yameshakamilika na wanategemea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye kuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo.
Pia, amebainisha kuwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo wamekuwa na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kongamano la wanawake wajasiriamali pamoja na midahalo ya malezi na makuzi.
“ Tofauti na shughuli tulizozifanya siku ya kilele tutakuwa na mambo mengine mengi ikiwemo kupima saratani ya shingo ya kizazi,elimu ya lishe,kupinga ukatili na mabanda mbalimbali ya maonesho,” amesema.
Madhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake wilayani humo yatafanyika katika Kata ya Makere na watu wote mnakaribishwa kuudhuria tukio hilo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.