Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa utumiaji wa majiko matawi utasaidia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya mkaa na kuni kitu kitakachopelekea uharibifuu wa mazingira uliokithiri kupungua.
Hayo yamebainishwa leo na Diwani wa Kata ya Rusesa iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu,Fabiano Dolagi alipokuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Majiko Sanifu katika kata hiyo mradi unaofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la NSV.
“Jiko Matawi ni jiko zuri linasaidia kutunza mazingira kwakuwa linatumia mkaa na kuni kidogo,gunia moja la mkaa mtu anaweza kulitumia hadi miezi mitatu ambapo siku za nyuma gunia moja mtu alikuwa analitumia wiki moja au mbili hivyo majiko haya ynatupeleka katika uchumi mzuri,” amesema.
Aidha,Dolagi ameishukuru Divisheni ya Maendeleo ya Jamii katika halmshauri hiyo kwa kuiteua kata anayoiongoza kuwa mojawapo ya kata mbili mradi huo utakapoanza kutekelezwa kati ya 21 zilizopo.
Naye Mratibu wa Progamu ya Mabadiliko ya Tabia SNV Wilaya ya Kasulu,Rozalia Mushi amesema Ubunifu wa majiko hayo ni njia moajawapo ya kuunga juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kuihimiza jamii kuhamia kwenye nishati safi.
Afisa Maendeleo Mwandamizi Halmshauri ya Wilaya ya Kasulu, Subira Swai amesema kuwa majiko hayo yatapunguza gharama za nishati kwa familia pamoja na kuboresha afya zao hasa mama na mtoto kwa kuwapunguzia adha ya moshi unaotokana na matumizi ya nishati chafu.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Afisa Tarafa ya Buyonga, Paul Ramadhan alibainisha kuwa mradi huo utaenda kutatua tatizo la uharibifu wa mazingira kwa kupunguza matumizi makubwa ya kuni na mkaa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.