Imeelezwa kuwa Mkoa wa Kigoma umefanikiwa kupunguza ukubwa wa changamoto ya wasiojua kusoma na kuandika kutoka wanafunzi 54,500 mpaka 18,650 kupitia Programu ya Shule Bora.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Msaidizi Elimu, Mwalimu Paulina Ndigeza alipokuwa akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Elimu ngazi ya Mkoa na Halmashauri juu ya usimamizi wa vipaumbele vya ufundishaji na ujifunzaji kwa mwaka wa tatu wa programu ya Shule Bora leo Jumatatu Agost 5, 2024.
Paulina ameeleza kuwa programu hiyo imewawezesha kutoa mafunzo na kuwafikia walimu wote wa shule za Msingi kupitia Mfumo wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) na kuwawezesha kupanda kwa ufaulu kutoka 76.3% hadi 82.6%.
“Tumeweza kuona mwamko mkubwa sana haswa kwenye ufaulu wa mitihani ya darasa la saba, kwa mwaka juzi Mkoa wa Kigoma ufaulu wake uliku 76.3% lakini matokeo ya mwaka jana wanafunzi walifaulu kwa 82.6% kwahiyo unaona mabadiliko makubwa tumeweza kuyapata kupitia hii program ” Amesema.
Ameeleza kuwa kupitia mafunzo mbalimbali ya viongozi yamesaidia kuongeza maarifa na weledi kwenye kusimamia utawala bora kwa wale wanaowaongoza
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,Joseph Maiga amesema kuwa wanayo matarajio chanya kupitia programu hiyo kuwa itasaidia kuondoa mdondoko mashuleni.
Na kuongeza kuwa kupitia Shule Bora kumesaidia kuwaunganisha wazazi na Walimu kupelekea kushirikiana vyema kitu kilichosaidia uhakika wa chakula mashuleni.
Ameeleza kuwa katika mwaka wa tatu wa programu ya Shule Bora vipo vipaumbele ambavyo vitasaidia kuongeza ujuzi na umahiri kwa walimu hasa kwenye ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Hisabati na Kingereza
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.