Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Mhe. Eliya Kagoma leo Jumanne ameongoza kikao cha Baraza la madiwani lililojikita kuwasilisha taarifa ya utendaji kazi kwa ngazi ya kata katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2023/2024.
Ambapo madiwani, watumishi na wananchi walioudhuria kikao hicho walipata fursa ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo, Dkt. Semistatus H. Mashimba .
Akitoa salamu za ukaribisho Kagoma amebainisha kuwa baraza hilo linaishi kama familia kwa kila mjumbe kutoa mawazo yake pasipo kubaguliwa kama anatoka chama tawala au upinzani.
“Karibu sana Kasulu sisi Baraza la Madiwani tunaishi kama familia tuna kata 14 zinazoongozwa na chama tawala, kata 7 zilizo chini ya wapinzani, viti maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watano na viti maalumu wawili kutoka upinzani,” amesema.
Na kuongeza kuwa : “Lakini hapa huwezi kujua CCM ni nani na mpinzani ni nani sisi tunaishi hivyo na kama kuna jambo Mwenyekiti anatakiwa kushauriwa napokea ushauri kutoka kona zote,”.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dkt. Semistatus H. Mashimba alihaidi kulipa ushirikiano wa kutosha baraza hilo na kutaka wamtumie vizuri katika kutatua changamoto zao mbalimbali.
“Niseme mbele ya baraza lako Mwenyekiti najikabidhi kwenu nikiondoka vibaya ni nyinyi na nikiondoka vizuri ni nyinyi hivyo mnilee kuna mambo nimetoka nayo huko nilipotoka mna wajibu wa kuniweka katika mstari,”.
Naye Diwani wa Kata ya Asante Nyerere, Mhe. Julius Mpwehuka amesma kuwa kata yake imefanikiwa katika suala la chakula la mashuleni baada ya kuwaelimisha wazazi umuhimu wa kushirikiana na serikali katika kufanikisha jambo hilo.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Nyamnyusi aliishukuru serikali kwa namna inavyotatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa kujenga shule, vituo vya afya na zahanati pamoja na kurejesha ruzuku ya mbolea kwa wananchi.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.