Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka watendaji katika sekta ya afya kuacha kuwatoza faini wakinamama waliojifungulia nje ya vituo vinavyotoa huduma hizo ikiwemo kutowalipisha gharama za kadi za kliniki
Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo Ijumaa Julai 12,2024 katika Kata ya Makere na Nyakitonto zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu aliposimama kuongea na wananchi wakati wa mwendelezo wa ziara yake mkoani Kigoma.
“Ni marufuku kwa mtumishi yeyote wa afya kuthubutu kumtoza faini mama aliyejifungulia nje ya kituo kinachotoa huduma za afya pamoja na kuwalipisha kadi za kliniki kwa ajili ya mtoto…afisa yeyote atakayebainika kusababisha kero yeye atakuwa kero na hatua dhidi yake zitachukuliwa,” amesema.
Aidha,amehimiza wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na kufuatilia maendeleo ya wanachojifunza huko mashuleni ili kusaidia taifa kuzalisha wataalamu wa kada tofauti siku za mbeleni.
Tofauti na hayo kupitia ziara hiyo Dkt. Mpango ameelekeza halmashauri zote kote nchini kutilia mkazo sheria ndogo ndogo za utunzaji wa mazingira ili kuzuia uharibifu wake kwa watu wanaofanya vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua.
HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
Anuani ya Posta: S.L.P 97
Simu ya Mezani: +255-028-2810339
Simu: +255-028-2810339
Barua Pepe: ded@kasuludc.go.tz
Copyright ©2024 kasuludc . All rights reserved.